Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa
matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya
maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa
na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa
kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange. Ubalozi wa Ufaransa
umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao.
Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa
wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo
makundi ya vijana wanaowarushia mawe.
Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku
wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu
kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni
wa Ufaransa huko Zinder.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni