Jumatano, 21 Januari 2015

MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza Bweni lote la wanafunzi wasichana wa Shule ya Mpwapwa Sekondari ya wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma

MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza Bweni lote la wanafunzi wasichana wa
Shule ya Mpwapwa Sekondari ya wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ikiwemo
vifaa vyao vyote.
Wakiongea Shuleni hapo wanafunzi waliounguliwa na vifaa vyao Pregina
Sabasi na Pascana Mpagama wamesema Bweni lote wanaloishi wanafunzi 64
limeteketea kwa moto ulioanza saa 3 na Nusu  asubuhi.
Pascana amesema vitu vilivyoungua ni pamoja na Magodoro, Nguo, Vitabu,
Madaftari, na kila kitu kilichokuwa kwenye bweni hilo.
Wamesema chanzo cha moto huo bado hawajakijua pamoja na kuwa Mmoja wao
aliona Nyoka juu ya Dari kabla ya kushuhudia Nguo zilizokuwa juu ya
kitanda zikiteketea bila godoro kuungua na baada ya muda moto
ukasambaa kwa kasi kubwa na wao kushindwa kuokoa chochote.
Kwa Upande wake Mkuu wa shule hiyo Nelson Milanzi amesema kutokana na
moto huo kuzuka kwa ghafura walishindwa kuokoa kitu chochote.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Christopher Kangoye amesema mpaka sasa
bado hawajajua Gharama halisi ya hasara iliyopatikana japo wataaramu
bado wanaendelea na tathimini wakiwemo kamati ya ulinzi na usalama wa
Wilaya hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post