Jumapili, 4 Septemba 2016

VIWANDA VYA KUSASISHA DHAHABU CHUNYA VILIVYO KATIKA MAKAZI VYALALAMIKIWA




Ezekiel Kamanga,Chunya.

Wananchi wa kijiji cha Kibaoni wilayani Chunya mkoani Mbeya wanalalamikia  viwanda vidogo vidogo vinavyotumika katika kusafishia dhahabu kutoka kwenye mchanga kwa madai kuwa moshi wake umekuwa  ukiwasababishia kuwashwa kwenye koo,mafua yasiyo isha na vikohozi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa kibaoni wamesema kuwa kwa sasa wanahofia afya zao pamoja mifugo yao kutokana na madhara walioanza kuyapata tangu viwanda hivyo  viwekwe karibu makazi yao.



Oswad Mbuya  mkazi wa kijiji hicho cha kibaoni  alisema moshi huo unaotoka katika viwanda hivyo vya uchenjuaji  unawasababishia kupata na mafua ya mara kwa mara,vifua,pua kuwashwa na vikohozi visivyo isha hali inayowalazima kuondoka nyumbani mara tu  wanapoanza shughuli hiyo ya kuprosesi dhahabu.

Mkazi mwingine aliyezungumzia sula hili ni Rose Tuli  alisema ni kwa muda mfupi tu tukwisha anza kupata madhara na kwamba endapo wataendelea na shughuli hii kwa muda wa miaka kadhaa hatui hatima yetu itakuwaje kwani sasa vifua visivyoisha,mafua vikohozi  hata tukinywa dawa hatupati nafuu.

Sabina  Thomas alisema  wao tu wamekuwa wanaumwa viohozi,mafua,na vichwa hajui mifugo yao wanayoifuga inaathirika vipi kwani wanafuga kuku,ngombe,nguruwe na mbuzi na kwamba wanaomba wataalamu waangalizie huo moshi kama hautakuwa na madhara zai ya hayo maana wanaishi kwa wasiwasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha kibaoni Joshua Mlambalala amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wananchi ambapo alisema kuwa wao kama serikali wanasubiri tamko la nemki kwani wamiliki wa viwanda wanaruhusiwa kufanya shughuli hizo baada ya kuruhusiwa na watu wa mazingira kufanya ukaguzi.

Mlambalala alisema kuwa watu wa mazingira walishafika katika kijiji chake na kuchukua michoro kwa wawekezaji wa viwanda  na kuwapelekea michoro NEMC ili kuona jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi na kuwapa maelekezo.
Kwa upande wake  afisa usafi na  mazingira wilaya ya chunya Yohana Ngulukia alisema kuwa ni kweli viwanda hivyo vipo kwenye maeneo ya makazi ya watu na kwamba si kitu kinachokubali  na kwmba kwa kuondoa malalamiko hayo wao kama halmshauri wamekwisha tenga hekari 10 katika kata ya Itewe kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo ili kupunguza malalamiko hayo kutoka kwa wananchi.

Ngulukia amesema wananchi wawe na subira  kuhusu kuondolewa kwa viwanda hivyo katika makazi kwani walishawapatia maelekezo wamiliki wa viwanda kutengeneza namna ya kufanya moshi usisambae kwenye maeneo ya watu na kwamba wanamikakati ya kupeleka huduma ya umeme katika eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda na maji.

Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post