Vijiji vinne vyaWilaya ya Bahi Mkoani Dodoma vipo hatarini kukosa huduma ya mji safi na slama baada yamkazi mmoja kuchoma chanzo cha maji wakati akiandaa shamba la mboga. Vijiji hivyo ni Babayu,Asanje,Kongogo na Tinai ambapo chanzohicho cha maji kipo katika kijiji cha Kongogo ambacho kinahudumia vijiji vyote vinne Mayunga Shelebi alichooma chanzo hicho wakati akiandaashamba lake la mboga kijijini hapo.
“Ni bahati mbaya tu siyo kwa makusudi nilikuwa naandaabustani yangu ya mboga lakini nikashangaa moto umeshafika hadi katika chanzocha maji, kwani mimi na familia yangu pia mbona tunatumia maji haya haya nakumwagilia bustani yangu pia natumia maji haya sasa iweji nichome chanzo hikikwa makusudi”alisema mkazi huyo Mayunga Shelebi.
Wanakiji wa Kongogo walilalamikia uharibifu huo wa chanzo chamaji na kudai kwamba Mayunga ana tabia ya ubabe na uonevu na inawezekana amechoma moto kwamakusudi chanzo hicho. “Tunaiomba serikali itusaidie kutokana na ubabe na uonevuambao umekuwa ukifanywa na mkazi huyu kwani tumechoshwa na vitendo vyake hivyovya kibabe “alisema Juma Mazengo.
“Tulipata shida ya huduma ya maji safi na salama kwa mudanrefu sana wafadhili kwa kushirikiana na serikali wakatupatia huduma hiyo yamaji halafu mtu anakuja kuchoma chanzo ch maji kwa makusudi ili kuturudishakatika shida ya maji tuliyokuwa nayo huko nyuma”alisema Eliasi Matonya.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kongogo Daudi Hussein alisemaalipopata taarifa hizo kutoka kwa wanakijiji alikwenda eneo la tukio na kukutachanzo hicho kimechoma,ambapo Mtendajiwa kijiji hicho Rashid Mhawi alisema alichukua hatua ya kumkamaka Mayunga na kumuwekarumande ili kumchukulia hatua zaidi. Hata hivyo Mayunga alikiri kosa lake
nakulazimika kulipa faini ya ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja ili kufidi uharibifuhuo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni