Jumapili, 18 Januari 2015

MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal amesema kiongozi Bora ambaye watanzania wanatakiwa kumchagua ni yule Mwenye hofu ya Mungu na si vinginevyo



MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal amesema kiongozi Bora ambaye
watanzania wanatakiwa kumchagua ni yule Mwenye hofu ya Mungu na si
vinginevyo.
Makamu huyo ameitoa kauli hiyo wakati wa kumsimika Askfu mteule wa
jimbo kuu katoriki la Dodoma Beatus Kinyaiya aliyeteuliwa kushika
nafasi hiyo baada ya aliyekuwa askofu wa jimbo hilo John nyaisonga
kuhamishiwa jimbo la mpanda.
Dkt Bilal amesema huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo waumini pamoja na
viongozi wa Dini zote nchini wanatakiwa kujuakua kiongozi mzuri ni
yule anaemcha mungu na ndiye anatakiwa kuchaguliwa.
Amewataka wananchi kujiepusha na watu wasiomcha Mungu kwani wao
wanataka kupata uongozi kupitia migongo ya wanyonge kwa malengo ya
kujinufaisha wao.
Aidha Dkt Bilal amewataka viongozi wa Dini zote nchini kuwafundisha
waumini wao kuishi kwa kuheshimiana na si kukashifiana katika Dini
maana kwa kufanya hivyo ni kuivunja katiba ya nchi na serikali
haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria.
Amesema kumuacha mtu anayeleta chokochoko za kidini ni kukribisha
uvunjifu wa Amani ya nchi ambayo ikipotea kuirejesha kwake ni ni kazi
kubwa na tena inaweza isirudi.
Viongozi mbalimbali wa Kiserikali walimehudhuria hafura hiyo ni pamoja
na Waziri Nchi Sera na uratibu wa Bunge Williamu Lukuvi, Waziri wa
Mambo ya Ndani Patrice Chikawe, Rais Wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa
na Mkewe, Spika wa Bunge Anna Makind, Mkuu wa Mkoa waDodoma Chiku
Gallawa pamoja na wakuu wa mikkoa ya Njombe na Singida wakiwemo wakuu
wa wilaya za Dodoma na maaskofu wa katoriki wa mikoa mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post