Baraza
la maadili ya utumishi wa umma limeshindwa kumuhoji mbunge wa Bariadi
Magharibi Mh Endrew Chenge baada kuwasilisha zuio la mahakama kuu
lililozua kutokuendelea kujadili miamala ya Escrow huku wanasheria wa
sekretarieti ya baraza hilo wakipingana naye kwa madai kuwa wao
wanajadili ukiukwaji wa maadili na siyo miamala ya Escrow.
Kufuatia
hali hiyo mwenyekiti wa baraza hilo jaji mstaafu Hamisi Msumi
ameahirisha kikao hicho hadi Feb 26 mwaka huu ili wajumbe wapate muda wa
kupitia zuio hilo ambapo baraza litakuja na uamuzi ama wa kuendelea au
kusitisha hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi wa sakata hilo.
Akisoma
hati ya malalamiko dhidi ya Chenge, mwanasheria wa sekretarieti ya
maadili, Hassan Mayunga amesema mlalamikiwa amekiuka maadili ya viongozi
wa umma ambapo akiwa mwanasheria mkuu wa serikali AG mwaka 1995
aliishauri serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na kampuni ya
Independent Power Solution Limited IPTL wa kuongeza uzalishaji wa umme.
Aidha
ameongeza kuwa wakati anafanya hayo hakuweka wazi kuwa ana maslahi
binafsi na baada ya kustaafu wadhifa huo Desemba 2005 aliingia mkataba
wa kuwa mshauri mwelekei wa kampuni ya Vip Engineering and Marketing
Limited iliyokuwa na hisa asilimia 30 kwenye kampuni ya IPTL kitendo
ambacho ni ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma ambalo
linamzuia kiongozi wa umma kujinufaisha na utumishi wake uliopita.
Akitetea
hoja yake ya kutaka baraza hilo lisitishe zoezi la kumuhoji Mh Chenge
amesema malalamiko dhidi yake ni chimbuko la uamuzi wa bunge na kutaka
apewe mwongozo wa suala hilo kuendelea kujadiliwa wakati mahakama kuu
imeshazuia huku akilitaka baraza hilo kutokuingia kwenye misukumu ya
kisiasa badala yake wafuate sheria za nchi na kukabidhi hati hiyo kwa
mwenyekiti wa baraza.
Hata
hivyo mara baada ya kutoka nje ya ukumbi waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari walipotaka kufanya naye mahojiano juu ya suala
hilo Mh Chenge majibu yake yalikuwa hivi.
Mwenyekiti
wa baraza hilo jaji mstaafu Hamisi Msumi akizungumza mara baada ya
kuahirisha zoezi hilo amesema amelazimika kufanya hivyo ili wapate fursa
ya kupitia zuio hilo ili kila upande uweze kupata haki.
Kwa
upande wa wanasheria wa sekretarieti ya baraza hilo wamepinga hoja
alizotoa mh Chenge na kudai kuwa wao walipitia zuio hilo na kufanya
uchunguzi wa kina kabla ya kumuta na awali walishafanya naye mahojiano
lakini hakutoa hoja hizo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni