Jumamosi, 2 Aprili 2016

KUTANA NA HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA ZA LEO APRIL 02.2016


ZANZIBAR


Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watu wanne wakiwemo vigogo wa Chama cha Wananchi CUF wakituhumiwa kupanga na kuhusika katika uratibu, utengenezaji na ulipuaji wa mabomu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishina Msaidizi wa polisi Salum Msangi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya upelelezi wa
kisayansi wa Polisi huku akisema wengine ni viongozi wa juu wa CUF ,wasomi na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar ambapo lengo lao lilikuwa ni kulipua makazi ya Makamu Wa pili na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar .

Watuhumiwa waliokamatwa ni Omar Bakari Nassor,Hassan Omar Issa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Magharibi Salehe Mohamed Saleh Katibu wa CUF Magharibi na Suleiman Mohmaed Bakari Katibu wa CUF Mfenesini.

Mkuu huyo wa upelelezi amesisitiza na kutoa onyo kuwa Jeshi la Polisi halitasita na linaendelea na kazi ya kuweka ulinzi kwa wananchi na yeyote au kikundi kitakachojaribu kuleta fujo polisi imejiandaa kikamilifu.


MALUNDE1/DENICE                  


 &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

 DAR ES SALAAM

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam limefanya usafi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kudumisha ushirikiano.

Usafi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi,Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Muhimbili,  Bi.Agnes Mtawa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO  Mhandisi Cyprian Luhemeja .

Usafi huo umefanyika katika maeneo yote muhimu ya Hospitali ikiwemo utoaji wa maji taka .

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo,  Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amesema zoezi la kufanya usafi halina budi kuwa endelevu ili kuhakikisha maeneo yote yanakua safi lakini pia kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtawa amewashukuru DAWASCO kwa uamuzi wao wa kufanya usafi hospitalini hapo ambapo ametumia fursa hiyo  pia kuwaomba wafanyakazi wa Shirika hilo kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wanahitaji damu.


FULLSHANGWE/DENICE                                                  

 &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

MOROGORO

Wananchi wa kijiji cha Dete kata ya Tununguo wilayani Morogoro wamemtaka mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Stephene Kebwe kufika kijijini hapo kujionea utendaji kazi wa askari polisi wa kituo cha Ngerengere.

Ombi hilo limekuja kufuatia mtu mmoja kuuawa kikatili na watu wasiojulikana bila askari wa kituo hicho kutoa msaada wowote kwa wananchi.

Wakizungumza wakati wa kuuondoa mwili wa marehemu Abas Mwarabu aliyekutwa porini akiwa amefariki na kubaki fuvu na mifupa kutoka na kuchukua muda mrefu tangu alipo uawa wananchi hao wamesema endapo askari wa kituo hicho hawataondolewa wataandamana hadi kwa mkuu wa wilaya kupinga utendaji kazi wa askari wa kituo hicho.


ITV/DENICE                                                                           

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&& 


KIGOMA
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayoendelea mjini Kigoma, imemtia hatiani David Kafulila na kumtaka kulipa gharama kutokana na kukiuka kanuni ya kuwasilisha hati za kiapo mahakamani, zikiwa zimethibitishwa kama Sheria ya Makosa ya Uchaguzi inavyoelekeza.


Hata hivyo, kiwango cha faini anachotakiwa kulipa hakikutajwa ambapo pia kosa hilo halikuzuia ushahidi wake kupokewa upya mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo aliyoifungua kupinga ushindi wa Hasna Mwilima  wa CCM kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, Kafulila aliyegombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi analalamika kupokwa ushindi.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mwilima ambaye ni mshtakiwa namba moja wakati msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni washtakiwa namba mbili na tatu.

Jaji wa Mahakama Kuu, Ferdinand Wambali amesema Kafulila aliwekewa pingamizi na mawakili wa utetezi wakimlalamikia kuwasilisha hati ya kiapo iliyokiuka kanuni za uwasilishwaji kwa mujibu wa sheria.

Jaji Wambali amesema Kafulila hakutekeleza matakwa ya kisheria ambayo yanaagiza anayewasilisha haki za viapo kuhakikisha kuwa zimethibitishwa kabla, kwa ajili ya shahidi kuanza kutoa ushahidi wake.


HABARI24/DENICE                                                                            

 ******************************************************************

HABARI ZA KIMATAIFA

GARISSA

Raia wa Kenya leo wameshiriki kumbukumbu ya kwanza ya shambulizi la kigaidi lililosababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika chuo kikuu cha Garissa.

Leo hii kundi la watu 100 wakiwa wamevalia fulana zenye ujumbe wa amani walikusanyika mjini Garissa, umbali wa kilometa 365, kaskazini mashariki mwa jiji la Nairobi kwa lengo la kushiriki ibada ya kuwakumbuka wahanga wa mkasa huo.

Katika eneo hilo Mbunge wa Garissa Aden Duale amenukuliwa na AFP akisema wapo pamoja na wazazi, na wanawataka kuwaeleza kwamba kwa pamoja kama taifa lazima wakabiliane na ugaidi.

Tarehe kama ya leo mwaka uliopita watu wanne wenye silaha, kutoka kundi la Al-Shabaab walikizingira chuo hicho, na kuwafyatulia risasi wanafunzi wakiwa katika mabweni na kuwauwa wengine katika makazi yao.

DWSWAHILI/DENICE                                                                     


 &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

WASHINGTON DC

Rais Barack Obama wa Marekani amesema takribani mataifa 102 yameridhia mkataba wa ulinzi wa malighafi za nyuklia na ana matarajio ya kuanza kutumika kwake hivi karibuni.

Aidha kiongozi huyo ameuonya mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu nyuklia, unaofanyika nchini mwake kwamba wenye itikadi kali kutoka Kundi la Dola la Kiislamu "wanawazimu" hawawezi kusita kutumia shambulizi hatari la kinyuklia.

Kwa matumani ya kufanikisha hatua za kimataifa kudhibiti makundi ya wenye itikadi kali kumiliki silaha za nyuklia au malighafi za kile walichoiita "bomu chafu," Obama  alichora taswira yenye kuonesha mfano wa maangamizi ya ulimwengu kutokana na athari ya shambulizi la nyuklia la kigaidi.

Obama ambae anamaliza muda wake wa uongiozi mwezi Januari mwakani, amekuwa mwenyeji wa mkutano wa nne na yumkini ukawa  wa mwisho wa viongozi wa mataifa wenye lengo la kupunguza hatari za kutokea maangamizi ya nyuklia.


DWSWAHILI/DENICE                                                                     

 &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

 NEWYORK
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kuweka mikakati ya kuwatuma wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ambapo vita vya kisiasa vilivyochukua takriban mwaka mmoja vinatishia kuwa vita vya kikabila.
Azimio hilo lililowasilishwa na Ufaransa limeutaka Umoja wa Mataifa kuweka mpango madhubuti wa kuwatuma maafisa wa kurejesha amani kwa ushirikiano na serikali ya Burundi.
Hata hivyo rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amepinga hatua yoyote ya kuingilia kati Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na robo milioni kutafuta hifadhi katika mataifa jirani tangu kuzuka kwa vurugu hizo mwaka uliopita.



DWSWAHILI/DENICE                                                                     

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post