Na Peter Mkwavila,Kongwa .
WATANZANIA
na Wadau mbalimbali wa elimu wameshauriwa kuchangia kwa kiasi kikubwa
kwa hali na mali na nguvu zao,juu ya upatikanaji wa madawati mashuleni
,ili kuwaondolea kero ya wanafunzi ya kukaa chini badala ya suala hilo kuiachia serikali kufanya peke yake.
Ushauri huo umetolewa na mdau wa elimu ambaye pia mkazi wa kijiji cha Tubugwe Saimon
Binde wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa madawati 63 kwa mkuu wa
wilaya hiyo Bituni Msangi kwa ajili ya shule ya msingi ya Tubugwe
Kibaoni iliyopo wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma jana.
Alisema
kutokana na hadha wanayoipata wanafunzi mashuleni ya kukaa chini juu ya
ukosefu wa madawati ,watanzania na wadau wa elimu tunastahili kuelekeza nguvu zetu katika kuchangia hali na ili kwa ajili ya kuisaidia serikali ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi ya kuliondoa tatizo hilo.
Alisema
kuwa hatua ya kuchangia msaada huo wa madawati kwa upande wake ni
pamoja na kuwafanya wananfunzi wa shule hiyo ili waweze kufanya vizuri
katika taaluma ya elimu ambayo kwa hivi sasa imekuwa ni vigumu kuipata
kutokana na walio wengi wamekuwa wakikaa chini.
“Mimi
kama mzazi nimeona nisaidiane na serikali ya awamu hii ya tano ambayo
imesema inataka kuhakikisha watoto wote kwenye shule zetu hakuna mtoto
ambaye atakaye kaa chini kwa ajili ya kukosa madawati,ndiyo maana na
mimi nimeamua kuiunga mkono jitihada hizo la kuliondoa kero hiyo ya
ukosefu wa madawati mashuleni na watoto wetu waweze kufanya vizuri kimasomo.”alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya hiyo ya Kongwa Bituni Msangi aliwataka
wananchi wa kongwa kuunga jitihada zinazofanywa na serikali ikiwa na
pamoja kutumia nguvu zao zitaklazowezesha upatikanaji wa madawati badala
suala hili kuachiwa mikononi mwa serikali peke yake.
Alisema
juhudi hizo ni pamoja katika kusaidiana uvunaji wa miti inayotengenezwa
madawati kuhakikisha wanashirikia kikamilifu kwa kutumia nguvu zao na
hata kwa kutoa mali na fedha ili zoezi hilo liendane na kauli ya Rais
ambayo amesema mpaka mwezi wa sita hakuna mwanafunzi yoyote ambaye
atakayekaa chini kwa kukosa dawati.
Alisema
ili kuhakikisha hadhima hiyo inatekelezeka ni muhimu wananchi wa wilaya
hiyo wakiwemo na wadau wa elimu wakashirikiana kwa pamoja na
serikali,ili kuwaondolea wanafunzi kero hiyo ya kukaa chini ambayo
inayowasababishia watoto walio wengi kufanya vibaya masomo yao pamoja na
wengine kujikutwa wakipatwa na magonjwa.
“Ninawaomba
wadau wengine wajitokeze kama alivyojitokeza mwananchi huyo wa kijiji
hiki cha Tubugwe ambaye amejinyima na kutoa fedha zake kwa ajili ya
kuisaidia serikali katika kuondokana na kero hii ya watoto wetu ya kukaa
chini ambayo imeikubwa karibu shule nyingi hapa nchini”alisema,
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Tubugwe Kibaoni Hadija Mohamed alisema kuwa katika shule yake hiyo jumla ya wanafunzi 584 ambao ni wa darasa la kwanza hadi la saba na kwa upande wa watoto wa shule ya awali ni 128 ambapo jumla kuu ni 712.
Alisema wanafunzi wa shule ya msingi ambao kutoka darasa la kwanza hadi la saba wanaokaa kwenye madawati ni 200 na wanaokaa chini ni 384 na kwa wanafunzi wa shule ya awali
wote kwa upande wao wanakaa chini,kutokana na idadi hiyo kuwa kubwa ya
wanafunzi shule hiyo inahitaji jumla ya madawati zaidi ya 366 ili
kuondoa kero hiyo ya kukaa chini kwa wanafunzi hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni