Jumanne, 20 Januari 2015

IMETHIBITIKA KUWA MUNA OBIEKWE

Imethibitishwa kuwa nyota wa filamu Nchini Nigeria, Muna Obiekwe amefariki Dunia toka Nollywood Muna Obiekwe ambaye alifariki Dunia jana mchana katika hospitali ya Festac iliyopo mjini Lagos nchini Nigeria.

Muna Obiekwe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini kwa muda mrefu, ugonjwa ambao alifanya siri hata kwa wenzake wa karibu kipindi cha uhai wake. Imefahamika kuwa hali ya afya yake ilikuwa ikidhorota siku hadi siku kitu kilichopelekea kifo chake.

Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza kuhusu kifo cha staa huyo ni kwamba Muna Obiekwe alikimbizwa hospitali jana asubuhi baada ya kukutwa akitapika mfululizo nyumbani kwake lakini punde tu baada ya kufikishwa hospitali aliaga dunia.

Washirika wa Nollywood pamoja na wapenzi wa filamu zake Duniani kote. Mwenyezi Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post