Rais
Jakaya Kikwete ana mchango mkubwa kwenye maisha ya Rehela Chalamila aka
Ray C. Kwa kutambua hilo, Ray C anatarajia kumpa zawadi maalum kwa moyo
wake aliouonesha kuokoa maisha ya muimbaji huyo aliyewahi kuwa mtumiaji
wa dawa za kulevya.
Ray C amewaambia waandishi wa habari kuwa hana zawadi kubwa zaidi ya kumpatia JK zaidi ya kuandaa show kubwa na kumkaribisha kuwa mgeni rasmi.
“Kwa ukweli sina uwezo wa ukweli wa kumpa chochote kile,” alisema Ray C. “Lakini nachojua kitu alichoniambia ni kwamba ‘nitafurahi sana ukirudi kwenye muziki na utaendelea na shughuli yako’ nikamwambia ‘baba nitafanya hivyo,” aliongeza.
“Kwahiyo nimeweza kurekodi album nzima na ninategemea nifanye show kubwa sana ambayo nitamwita yeye awe mgeni rasmi na nina uhakika siku atakayoniona kwenye stage atajua kweli nimerudi, kweli aliokoa kipaji. Maana yake ameokoa kipaji, watanzania walishanizoeana na nadhani ningeondoka kwa style ile nadhani ningewaumiza sana mashabiki wangu. Nashukuru nimerudi ni ni mzima wa afya.”

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni