Mkuu wa kanisa katoliki nchini
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ameunga mkono maandamano ya kupinga
mabadiliko katika ya sheria ya uchaguzi ambayo imezua siku tatu za
maandamano.
Kadinali laurent Monsengwo ameitaka mamlaka kwa maneno yake mwenyewe kusitisha mauaji ya raia wake.
Amewataka waandamanaji kuweka amani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa zaidi ya watu 40 wamefariki katika ghasia hizo.
Vyama
vya upinzani vinasema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa ililenga
kuchelewesha uchaguzi ili rais Joseph Kabila aendelee kuwa mamlakani
baada ya kipindi chake cha utawala kuisha mwaka ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni