Kamanda mkuu wa kundi la waasi la
LRA nchini Uganda Dominic Ongwen amewasili mjini Hague ambako
atafunguliwa mashitaka ya uhalifu wa kivita.
Ongwen, alikuwa kamanda mwenye kuogopewa sana katika kundi la waasi
la LRA na alikamatwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mapema mwezi huu.
Uganda ilikubali kwamba muasi huyo apelekwe katika mahakama ya
kimataifa ya ICC, licha ya nchi hio kuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama
hio.
Wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wa Afrika, wamekuwa wakifanya msako dhidi ya Ongwen tangu mwaka 2011.
Anasemekana kua naibu wa kiongozi wa LRA Joseph Kony ambaye bado yupo mbioni.
ICC ilisema kwamba Ongwen atazuiliwa katika kituo kimoja nchini Uholanzi hadi mahakama itakapokuwa tayari kusikiliza kesi yake.
Alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu alipowasili Hague huku tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yake ikisubiriwa.
Taarifa ilitolewa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na
katibu mkuu wa umoja huo ikipongeza hatua ya kumpeleka Ongwen mjini
Hague.
Ban alisema ni hatua kubwa katika kuhakikisha kwamba waaathiriwa wa unyama uliotendwa na LRA wanapata haki.
‘Matumaini kwa waathiriwa’
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki pia
amepongeza hatua ya kukamatwa kwa muasi huyo akisema inatoa matumaini
makubwa kwa waathiriwa wa uasi wa kundi la LRA.
Tunawataka waasi wengine wa kundi la LRA waliosalia kufuata nyayo za
Ongwen na wapiganaji wengine wa kundi hilo waliojisalimisha tangu mwaka
2012, kusalimisha silaha zao na kurejea nyumbani.
Marekani sio mwanachama wa mkataba wa Roma uliosaidia kuundwa kwa
mahakama ya ICC lakini licha ya hilo, ilisaidia katika kumkabidhi muasi
huyo kwa ICC.
Awali ilitoa ahadi ya zawadi ya dola milioni 5 kwa yeyote ambaye angetoa taarifa kumhusu Ongwen na kupelekea kukamatwa kwake.
Anatuhumiwa kwa madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo kutumia waathiriwa kama watumwa.
Uasi wa LRA ulianza zaidi ya miaka 20 iliyopita kaskazini mwa Uganda
na inakisiwa kati ya wpaiganaji 200-500 wameteswa na waasi wa kundi hilo
nchini DRC, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni