WANAFUNZI wawili wa Darasa la tatu na tano wenye ulemavu wa kutosikia [viziwi] waliokuwa wanasoma katika shule ya msingi Dodoma viziwi iliyopo kisasa katika kata ya makulu wamefukuzwa shule baada ya kupata ujauzito.
Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Dodoma Agostino Kalinga amesema wanafunzi hao walipata mimba kutokana na kuruka uzio wa shule nyakati za usikuna kukutana na wanaume ambao ndiyo waliowapa huo ujauzito
Amesema baada ya kubainika kuwa na Mimba wamerudisha majumbani kwao ambapo mmoja ni mkazi wa Mvomelo Mkoani Morogoro na mwingine ni mkazi wa swaswa Dodoma.
Kalinga amewataka walimu wa shule hiyo maalumu ya kufundisha wanafunzi wenye uziwi 83 waliopo na shuleni hapo kuhakikisha wanakuwa karibu nao katika kuwaangalia na kuwasaidia ili kuwaepusha na hatari za vishawishi vinavyoweza kusababisha mimba zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni