Rapa anayechipukia Rymir Satterthwaite anasema Jay z ni baba yake mzazi
na anataka vipimo vya DNA. Kijana huyu mwenye miaka 21 anasema Jay Z
alikuwa na mahusioano na mama yake kwenye miaka ya tisini na kwamba
walikuwa pamoja kwa muda mrefu kabla hajawa maarufu.
Rymir anataka vipimo vya DNA Ila Jay z
hajakubali kufanya hivyo ndio maana mpaka sasa kijana huyu amechukua
hatua ya kwenda mahakamani kutaka mahakama ilazimesha vipimo hivyo.
Rymir analalamika kuwa ameishi kwenye maisha ya shida huku baba yake
akiwa tajiri kwa muda mrefu. Jay Z anajulikana kuwa na mtoto mmoja tu
ambaye ni Blue Ivy Carter na mke wake ambaye ni Beyoncé Knowles
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni