Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kitendo cha Mwenyekiti wa CCM,
Rais John Magufuli kuendelea na mikutano ya kisiasa mikoani na kuwazuia
viongozi wa vyama vingine vya siasa ni kutaka kukwamisha demokrasia
nchini.
Akizungumza
jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni ya Azam,
Mbatia alisema Rais Magufuli akiwa Singida, aliviponda vyama vya
upinzani kuwa vimekufa.
“Akiwa
Singida Magufuli alisema vyama vya siasa vya upinzani vimekufa na
kuvilinganisha na nyoka aliyekanyagwa kichwa na kubakiwa na mkia tu
unaocheza cheza,” alisema.
Alisema
Agosti 12, mwaka huu Magufuli alikuwa mtaa wa Lumumba, jijini Dar es
Salaam akizungumza na wanachama wake na kuonyeshwa na televisheni
mbalimbali akikijenga chama chake.
“Nani
anakwenda kuweka rekodi vizuri huko mikoani kwa anayoyasema Magufuli
kama anazuia wapinzani wasifanye siasa? Kwa hiyo yeye anajenga chama
chake lakini anazuia wapinzani wasifanye hivyo,” alisema.
Alisema ikumbukwe kuwa Tanzania ni ya watu wote na wanatakiwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa na si vinginevyo.
Msikilize hapo chini akiongea>>
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni