Wakati anazaliwa alipewa jina la Muhammad Yusuf Khan, alizaliwa mnamo december 11 mwaka 1922, lakini kwa sasa jina maarufu analojulikana ni Dilip Kumar ni msanii wa filamu za kihindi .
Alipata
kuoa mkewe ambaye yuko naye hadi hivi
sasa ajulikanaye kama Saira
Banu mnamo mwaka 1966
Asma (1979–1982) |
Kipindi chake cha uigizaji kimedumu kwa takribani miongo sita huku akicheza zaidi ya filamu 60.
Ameshiriki katika filamu zenye mafanikio kama vile Andaz (1949), Aan (1952), Devdas (1955), Azaad (1955), Mughal-e-Azam (1960) na Ganga Jamuna (1961).
Dilip Kumar amefanya kazi pia na mwana mama Vyjayanthimala akiigiza nae takribani filamu saba together zikiwemo zilizochezeka katika production kongwe ya Gunga Jamuna na kupata umaarufu zaidi.
Mwaka 1976, Dilip Kumar aliamua kupumzika kwa takribani miaka mitano na aliporejea alikuja kuigiza kama mhusika mkuu katika filamu ya Kranti (1981) na kuendelea kuwa mwigizaji kuu katika filamu za Shakti (1982), Karma (1986) na Saudagar (1991). Wakati filamu yake ya mwisho ilikuwa ni ile ya Qila (1998).
Ndie msanii wa kwanza kutwaa tuzo maarufu ya Filmfare Best Actor Award (1954) na bado anashikilia rekodi ya kutwaa tuzo hizo kwa wingi akiwa ameshinda tuzo nane.
Na hii inatoa maana ya msanii huyu kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini india.
Ikumbukwe kuwa serikali ya india ilipata kumzawadia tuzo ya Padma Bhushan mwaka 1991,[11] pia alipata tuzo ya Dadasaheb Phalke Award mwaka 1994 na Padma Vibhushan.
Ukiachana na mwaka 2015 kutajwa kuwania tuzo ya Rajya Sabha, moja kati ya tuzo nzuri kabisa katika bunge la nchini india.
Serikali ya pakistan ilimzawadia tuzo ya Nishan-e-Imtiaz mwaka 1997. civilian honour
Maisha yake ya awali
Baba yake Lala Ghulam Sarwar, alikuwa akimiliki ardhi na miti ya matunda huko Peshawar na Deolali (huko Maharashtra, India).Dilip Kumar alisomea katika shule ya Barnes School, Deolali, karibu na Nasik.
Miaka ya 1930s,familia ya watu 12 akiwemo Dilip ilihamia mjini Mumbai.
Miaka ya 1940, wakati akiwa bado katika amilia yao alikuwa na maelewano hafifu na baba yake , Dilip Kumar aliamua kuondoka nyumbani na kuelekea mjini Pune.
Kwa msaada wa mmiliki wa mgahawa mmoja wa kiiran Kumar alipat abahati ya kusaini mkataba na Taj Mohammad Shah, ambaye alikuwa ni rafiki wa baba yake kutokea Peshawar.
Alifanikiwa kupata kazi hiyo pasipo kupata msaada kwa familia yake kutokana na kuwa na uelewa mzuri wa kuzungumza na kuandika vema kiingereza.
Aliweza kuanzisha duka katika maeneo yale ya klabu ya jeshi na wakati mkataba kumalizika aliweza kurejea nyumbani kwao Bombay akiwa na kiasi cha Rupia 5000.
Namo mwaka 1942, aliamua kuanzisha baadhi ya miradi kwa lengo la kumsaidia baba yake kujikimu hasa katika upande wa kodi ya nyumba.
Alikuja kukutana na Dr. Masani pale Churchgate Station, ambaye alimuomba kumsaidia kupata kazi katika kampuni ya Bombay Talkies huko Malad. Na hapa ndipo alipokutana na mwanadada Devika Rani, mmiliki wa Bombay Talkies, na kumtaka Dilip kuingia mkataba na kampuni yake wa Rupia 1250 kwa mwezi.
Na hapa ndipo alipokutana na msanii Ashok Kumar ambaye alivutiwa na uigizaji wake na kumwambia anapaswa kuigiza kialisia.
Pia akiwa hapo alikutana na mwigizaji Sashadhar Mukherjee, na wote hawa wakawa karibu sana na Dlip kwa miaka mingi.
Kiufupi Kumar alisaidiwa jinsi ya kuandika story za filamu na miongozo ya filamu kwa sababu alikuwa amebobea katika lugha ya kihurdu.
Devika Rani alipendekeza kubadilisha jina lake kutoka kuitwa Yousuf kwenda kuitwa Dilip Kumar, na baadae akamjumuisha katika filamu ya Jwar Bhata (1944),akimtaka kuongoza filamu hiyo kama mhusika mkuu nah ii ndio ilikuwa filamu iliyoanza kumtambulisha dilip katika ulimwengu huu wa Indian cinema ndani ya Hindi film industry.
KIPINDI CHA MIAKA YA 40
Miaka y a 1940 Dilip Kumar alitoka na filamu za Jwar Bhata (1944) , Jugnu (1947) Shaheed {1948}. Andaz (1949) akiicheza na Raj Kapoor pamoja nae Nargis.Miaka ya 1950 alitoa movie nyingine nyingi ambazo nazo zilifanya vema baadhi ni kama vile Jogan (1950), Tarana (1951) Hulchul (1951) Deedar (1951), Daag (1952), Devdas (1955), Yahudi (1958) and Madhumati (1958),Amar (1954).Footpath (1953), Naya Daur (1957), Musafir (1957) and Paigham (1959). Kama nilivyokwambia hapo mwanzo, alikuwa ni msanii wa kwanza kushinda Filmfare Best Actor Award kupitia filamu ya Daag na kuendelea kushinda mengine saba .
Ameweza pia kufanya vizuri katika filamu zake akiwa na waigizaji wa kike mfano ni Madhubala, Vyjayanthimala, Nargis, Nimmi, Meena Kumari, na Kamini Kaushal.
Mnamo mwaka 1960 alicheza filamu ya Prince Salim ambayo mwaka 2008 ndio ilitangazwa kuwa filamu ya pili kwa mauzo ya juu ya filamu za nchini india katika historia.
Filamu ilikuwa ikimuelezea mwana mfalme ambaye alimmpindua baba yake katika utawala ,pia filamu hii ilichezwa na Prithviraj Kapoor) na kujikuta akizama kwenye penzi la binti aliyekuwa akijiuza nafasi hii ikichezwa na {Madhubala).
Filamu hii kwa eneo Fulani ilikuwa ina rangi ya kizamani {black and white},isipokuwa baadhi ya maeneo ndio yalikuwa na rangi.
Lakini miaka 44 baada ya original kutoka ikatoka sasa nyingine yenye mwonekano wa kileo { fully colourized} ikaachiwa mwaka 2004.
Miaka ya sitini pia alitoa filamu In Lawrence of Arabia (1962), Leader (1964),Dil Diya Dard Liya,Ram Aur Shyam na Aadmi.Pia amecheza filamu ya Dastaan (1972) na Bairaag (1976, Gopi (1970), Sagina Mahato (1970) na Bairaag (1976).
Mwaka 1981,alirejea na filamu ya Kranti ambayo ilikuwa ni boya ya mwaka huo.
Katika filamu hiyo alicheza na mastar Manoj Kumar, Shashi Kapoor, Hema Malini na Shatrughan Sinha,
ZAWADI
Dilip Kumar duniani kote anafahamika kwa movie za kihindi. Ameingia pia kwenye record katika kitabu cha Guinness World Record kwa kushikilia tuzo nyingi akiwa ni msanii kutoka India.zikiwemo 8 za Filmfare Best Actor awards na mara 19 za kutajwa kuwania kushindania tuzo tofauti tofauti pia akipokea tuzo ya Filmfare Lifetime Achievement Award ya mwaka 1993.Serikali ya india pia ilimpatia tuzo maarufu ya serikali ijulikanayo kama Padma Bhushan mwaka 1991, pia akapokea ya Dadasaheb Phalke mwaka1994 pamoja na Padma Vibhushan mwaka 2015.
Tuzo yake kubwa nay a kimataifa aliipata mwaka 2009 ya CNN-IBN Lifetime Achievement Award.
Huyo ndiye DIllip Kumar……………birthday yake ilikuwa siku ya jumamosi iliyopita akifikisha miaka 94 mwezi disemba 11.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni