
Mwanamuziki wa Malaysia Namewee
Polisi wamemkamata
mwanamuziki maarufu wa kutatanisha wa Malaysia baada ya malalamiko
kutoka kwa raia kuhusiana na wimbo wake wa hivi karibuni unaokisiwa
'kuwatusi waislamu'
Namewee, 33, ambaye jina lake rasmi ni Wee
Meng Chee alikamatwa siku ya Jumapili katika uwanja wa ndege wa Kuala
Lumpur huko Malaysia. Video hiyo kwa jina Oh My God, ambayo inadaiwa kuudhi, ilizinduliwa rasmi mwezi Julai ambapo mwanamuziki huyo anaonekana akiimba kwa kutumia mtindo wa kufoka mbele ya msikiti nchini Malaysia.

Polisi wamesema wamemkamata na atazuiliwa kwa siku nne kuchunguza iwapo mwanamuziki huyo 'aliichafua' sehemu hiyo ya maombi kimakusudi ili kuitusi dini hiyo.
Akipatikana na hatia, huenda akafungwa jela hadi miaka miwili
Takriban robo tatu ya raia wa Malaysia ni Waislamu, ingawaje kuna dini kama vile za Kikristo, Kihindu na Kibudha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni