Alhamisi, 1 Septemba 2016

CHUKUA HATUA SEPTEMBA MOSI 2016


Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.


Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.

Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitawasaidia vijana kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.

Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.

Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.

Kipindi kimeanza kuruka hewani kwa mara ya kwanza leo Alhamisi kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.

na hiyo ndio sehemu ya kwanza au ufunguzi wa kipindi hicho zaidi vijana na viongozi wakizungumzia kuhusu maana halisi ya Chukua Hatua......

Pia unaweza kusikiliza kupitia #kazenzele1.blogspot.com, #domfahari.blogspot.com, pia katika ukurasa wa Facebook wa Rasi fm radio.

>>>Sikiliza hapa chini >>> 
 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Ad Inside Post