NA: Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wananchi
na viongozi wa kijiji cha kiwanja kata ya mbugani wilayani Chunya
Mkoani Mbeya wameaswa kujenga mahusiano mazuri na wawekezaji wanaofika
kijijini kwao ili kuleta maendeleo katika kijiji.
Haya yameelezwa na Afisa Mazingira Taifa Paul Kalokola wakati akizungumza na viongozi wa kijiji pamoja na wajumbe kijijini hapo mara alipofika kufanya ukaguzi kwenye eneo la Mwekezaji wa madini ya dhahabu Aidan Msigwa aliyewekeza kijijini hapo.
Ambapo alieleza kuwa kama
muwekezaji ameonyesha nia ya kuwekeza ni vyema na wao wampatie
ushirikiano wakutosha kwani kupitia yeye vijana wengi wanaweza kupata
ajira na kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Kalokola
aliendelea kueleza kuwa lengo la wao kufika kwa hapo ni kukagua na
kujua mahusiano yaliopo kati muwekezaji huyo na wananchi ili kujirisha
pindi wanapo mpatia hati ya kuendesha kampuni yake.
Kwa upande wake Mtendaji wa kata hiyo ya mbugani Sadick Kaulule aliwataka maofisa wa mazingira kuwa utaratibu wa kuwatembelea wananchi pamoja na wawekezaji wengine kama walivyofanya ili kuondoa migogoro inayoweza kuepukika kutokana na wananchi kuhofia baadhi ya wawekezaji wanaojishughulisha na uchenjuaji wa madini kwa kutumika kemikali kwania ya kuwatoa hofu miongoni mwao.
Pia aliwashukuru kwa kufika kwao kueleza wao kama vingozi hawana pingamizi lolote kuhusu muwekezaji huyo kuwekeza kijijini kwao kwani amekuwa msaada katika jamii nzima kutokana na kutoa ajira kwa vijana kama wanampatia hati hawezi kuizuia.
MWISHO.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni